• HABARI MPYA

  Monday, May 16, 2022

  SIMBA NA YANGA MEI 28 KIRUMBA NUSU FAINALI ASFC


  NUSU Fainali za Kombe la Shirikisho Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu Arusha na Mwanza.
  Nusu Fainali ya kwanza baina ya watani wa jadi, Simba ambao ni mabingwa watetezi na Yanga itachezwa Mei 28 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, wakati ya pili itafuatia Mei 29 baina ya Azam FC na Coastal Union Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Mwaka jana Simba waliifunga Yanga katika fainali 1-0 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, bao pekee la kiungo Mganda, Thadeo Lwanga.
  Fainali ya mwaka huu itafanyika Julai 2 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA MEI 28 KIRUMBA NUSU FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top