// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NI COASTAL NA YANGA FAINALI ASFC, AZAM YAFA KWA MATUTA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NI COASTAL NA YANGA FAINALI ASFC, AZAM YAFA KWA MATUTA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Sunday, May 29, 2022

  NI COASTAL NA YANGA FAINALI ASFC, AZAM YAFA KWA MATUTA


  TIMU ya Coastal Union ya Tanga imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa penalti 6-5 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Sasa Coastal, mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mwaka 1988 watakutana na Yanga katika Fainali Julai 2, mwaka huu hapo hapo Sheikh Amri Abeid.
  Waliofunga penalti za Coastal ni Muhsin Makame, Amani Kyata, Paschal Kitenge, Abdul Suleiman, Willy Kisingi na Mbaraka Hamza, wakati Miraj Hassan alipiga juu ya lango.
  Kwa upande wa Azam waliofunga ni Rodgers Kola, Bruce Kangwa, Never Tigrere, Aggrey Morris na Idris Mbombo, wakati ya Lusajo Mwaikenda iliokolewa na kipa Mohamed Hussein huku Charles Zulu akipiga juu.
  Ikumbukwe jana Yanga iliwatoa mabingwa watetezi, Simba kwa kuwachapa 1-0, bao la Feisal Salum Abdallah dakika ya 25 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI COASTAL NA YANGA FAINALI ASFC, AZAM YAFA KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top