// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MO DEWJI ATAKA SIMBA ISUKWE UPYA IREJESHE MAKALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MO DEWJI ATAKA SIMBA ISUKWE UPYA IREJESHE MAKALI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Saturday, May 28, 2022

  MO DEWJI ATAKA SIMBA ISUKWE UPYA IREJESHE MAKALI


  RAIS wa heshima wa Simba SC, Mohamed 'Mo' Dewji amesema timu inahitaji kusukwa upya ili kurejesha makali.
  Kauli hiyo inafuatiwa timu kutemeshwa Kombe la shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kutolewa katika Nusu Fainali.
  Mo Dewji ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram mara tu baada ya pambano dhidi ya watani, Yanga jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, Simba ikichapwa 1-0 bao la kiungo Mzanzibar, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' dakika ya 25
  "Hogereni watani! Huu umekuwa msimu mbaya zaidi kwa Simba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Bodi inahitaji kufanya maamuzi magumu juu ya njia ya kusonga mbele. Tunahitaji kurekebisha timu kwa mkakati wa kurudi kwenye matokeo mazuri. Tulikosa ari na kiu ya kushinda mataji mwaka huu,"amesema Mo.
  Tayari Simba imekwishapoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, kutokana kuachwa mbali na watani wao hao, Yanga.
  Ikumbukwe mapema mwanzo wa msimu Simba ilivuliwa Ngao ya Jamii na Yanga baada ya kuchapwa 1-0.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MO DEWJI ATAKA SIMBA ISUKWE UPYA IREJESHE MAKALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top