• HABARI MPYA

  Monday, May 23, 2022

  CAMEROON HAWAKUAMINI ALIYEPIGA HAT TRICK NI BINTI


  MAAFISA wa Cameroon jana wamedaiwa kumkagua jinsia yake mshambuliaji wa Tanzania, Clara Luvanga ili kujiridhisha ni mwanamke kabla ya mchezo wa kwanza Raundi ya mwisho kufuzu Fainali za Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya umri wa miaka 17.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé, Serengeti Girls ilishinda 4-1, huku Clara anayechezea Yanga Princess akipiga hat-trick kwa mabao yake ya dakika za 29, 63 na 71 baada ya Diana William kufunga la kwanza dakika ya tatu, wakati na la wenyeji likifungwa na Mona Lamine dakika ya 26.
  Pongezi kwa maafisa wa Tanzania walioambatana na timu hiyo kwa kumjenga kisaikolojia Clara pamoja na udhalilishaji huo aliofanyiwa, adha kama ambayo aliwahi kuipata mwanariadha wa Afrika Kusini, Caster Semenya ambaye baadhi wa watu walikuwa wanamtazama Caster kama mwanaume, sio mwanamke.
  Timu hizo zitarudiana wiki ijayo Zanzibar, Serengeti Girls ikihitaji kuulinda ushindi wake ili kwenda India.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON HAWAKUAMINI ALIYEPIGA HAT TRICK NI BINTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top