• HABARI MPYA

  Sunday, May 22, 2022

  SERENGETI GIRLS YATANGULIZA MGUU MMOJA KOMBE LA DUNIA


  TANZANIA imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, Cameroon katika mchezo wa kwanza Raundi ya mwisho kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Wasichana chini ya umri wa miaka 17, baadaye mwaka huu nchini India.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé, mabao ya Serengeti Girls yamefungwa na Diana William dakika ya tatu na Clara Luvanga mengine yote matatu dakika za 29, 63 na 71 huku la wenyeji likifungwa na Mona Lamine dakika ya 26.
  Timu hizo zitarudiana wiki ijayo Dar es Salaam, Serengeti Girls ikihitaji kuulinda ushindi wake ili kwenda India.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI GIRLS YATANGULIZA MGUU MMOJA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top