• HABARI MPYA

  Tuesday, May 17, 2022

  GEITA YAIDIDIMIZA MBEYA KWANZA SONGEA

  MSHAMBULIAJI George Mpole amefunga bao la 13 la msimu, timu yake Geita Gold ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Maji Maji Jijini Songea mkoani Ruvuma.
  Mpole alifunga bao hilo pekee dakika ya 12 na kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 34 na kupanda nafasi ya nne, ikizidiwa pointi mbili na Namungo FC baada ya wote kucheza mechi 24.
  Mbeya Kwanza hali inazidi kuwa tete baada ya kichapo cha leo, ikibaki na pointi zake 21 za mechi 24 na sasa inashika mkia kwenye ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA YAIDIDIMIZA MBEYA KWANZA SONGEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top