• HABARI MPYA

  Tuesday, May 17, 2022

  SIMBA SC YAPIGWA FAINI MILIONI 23 KWA USHIRIKINA


  SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limeipiga Klabu ya Simba faini ya dola za Kimarekani 10,000 zaidi ya Sh. Milioni 23.2 za Tanzania.
  Adhabu hiyo imetokana na Simba kufanya vitendo vya kishirikina kwenye ya marudiano Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Orlando Pirates Uwanja we Orlando Pirates Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
  Simba ilitolewa kwa penalti 4-3 baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani.
  Tayari Orlando Pirates imeingia Fainali baada ya kuitoa na Al Ahly Tripoli ya Libya kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 ugenini na kufungwa 1-0 nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAPIGWA FAINI MILIONI 23 KWA USHIRIKINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top