• HABARI MPYA

  Monday, May 30, 2022

  POLISI TANZANIA YAICHAPA BIASHARA 2-0 MOSHI


  WENYEJI, Polisi Tanzania wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Mabao ya Polisi Tanzania yamefungwa na Deusdedith Okoyo dakika ya na 31 na Tariq Seif dakika ya 41 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 33 na kusogea nafasi ya saba, wakati Biashara United inabaki na pointi zake 24 katika nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 26.
  Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitateremka daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YAICHAPA BIASHARA 2-0 MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top