• HABARI MPYA

  Wednesday, May 18, 2022

  BILIONI 1.2 ZA JACKPOT YA SPORTPESA ZAENDA KILUVYA

  KAMPUNI ya Michezo na Burudani SportPesa leo imemtambulisha rasmi mshindi wa Jackpot ya shilingi 1,255,316,060 Florian Valerian Massawe (36) kutoka Kiluvya, Dar es Salaam.
  Florian ni fundi makenika na amefanikiwa kuwa bilionea wa kwanza wa SportPesa baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 13 za Jackpot za wiki iliyoisha.
  Akimtambulisha mshindi huyo wa awamu ya nane mbele ya waandishi wa habari, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas alianza kwa kumpongeza Florian kwa ushindi wake na kuwa bilionea wa kwanza aliyetokana na kubashiri mpira wa miguu.


  Mshindi wa Jackpot ya SportPesa, Florian Valerian Massawe akikabidhiwa rasmi mfano wa hundi ya Tsh. 1,255,316,060 na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas (kulia)

  ''Leo ni siku ya furaha kwangu na kwa wafanyakazi wengine wote wa Sportpesa kwa kumpata mshindi wa Jackpot. Napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya kampuni kumtambulisha kwenu Florian Valerian Massawe kuwa mshindi rasmi wa Jackpot yetu akiwa amejishindia zaidi ya bilioni 1.2” 
  “Kwa bahati nzuri mshindi wetu amepatikana wakati tunasherehekea miaka 5 tangu kuanza shughuli hizi za michezo ya kubashiri hapa nchini Tanzania.Ushindi wa Florian umefanikisha dhamira yetu ya kuwawezesha na kuwainua watanzania kiuchumi na kutengeneza bilionea wa kwanza.
  “Nyote ni mashahidi leo kiwango hiki cha pesa alichoshinda ni kikubwa na kitainua maisha yake na familia yake na pia jamii ambayo anaishi nayo.”
  “Hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni yetu kuwa ya kwanza kumtangaza mshindi wa kiasi kikubwa(Bilioni 1.2) kwenye sekta ya michezo ya kubashiri ambaye leo anakabidhiwa hundi ya pesa aliyoshinda.


  Mshindi wa Jackpot ya SportPesa Tzs.1,255,316,060 Florian Valerian Massawe akishikilia mfano wa hindi baada ya hafla ya kukabidhiwa rasmi na SportPesa

  Niwaase tu watanzania huyu ni mshindi wa nane kati ya washindi wetu wa Jackpot ambao tayari wameshashinda huko nyuma. Napenda kuwakumbusha chezeni na Sportpesa ili muwe mabilionea hapa Tanzania.”
  Akizungumza kwa niaba ya TRA Mkuu wa kitengo cha michezo ya kubahatisha, Shabani Mwanga alimpongeza kwa ushindi alioupata wa zaidi ya bilioni 1 na pia kama mtanzania mzalendo amechangia kwenye uchumi wa nchi kwa kodi ambayo Imetokana na ushindi wake wa Jackpot.
  ''Kama mwakilishi wa TRA nimefarijika kwa ushindi wako na pia kwa mchango ambao umeutoa si kwa kiwango hiki tu cha bilioni 1.2 tu, bali hata kwa siku za nyuma ambazo umekuwa ukicheza na ukishinda.”
  “Kwa ushindi huu Florian amechangia jumla ya Tzs 188,297,109 kama kodi, ikiwa ni 15% ya makato katika pesa aliyoshinda ya Tsh 1,255,316,060 na hivyo atabakiwa na Tshs 1,067,018,951 kama faida yake”
  “Ni matumaini yangu utajitahidi kuwa mweledi katika michezo hii na pia kwa taifa lako kama ulivyofanya sasa''.
  Naye Mkurugenzi Mtendaji kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania (GBT) James Mbalwe alimpongeza Florian kwa ushindi na kumtaka kuendelea kuwa mwadilifu kwani pesa aliyoshinda ni nyingi hivyo zinaweza kumfanya akakengeuka.
  ''Nachukua nafasi hii kukupongeza kama ambavyo wenzangu waliotangulia walivyofanya na pia napenda kuwaasa watanzania kuamini bodi ya michezo ya kubahatisha.”
   Niwaambie sisi tupo nanyi siku zote kama ambavyo tumekuwa karibu na Sportpesa na makampuni mengine pamoja na wachezaji wenyewe. Leo kama mnavyoshuhudia tuko sambamba na tumeshuhudia hatua zote za kiuweledi katika hatua za kuthibitisha ushindi wake, hii ni katika kuweka imani kwa wachezaji kwamba fedha zenu pamoja na zawadi zenu ziko salama. 
  Kwa umri bado wewe ni kijana na hii pesa uliyoshinda ni nyingi tungependa uwe mfano  mwema kwa wengine kwa kufanya yale yenye manufaa kwako na kwa familia yako. 
  Akitoa neno la shukrani kwa Sportpesa Florian anasema kwanza kwake imekuwa ndoto ambayo imetimia katika muda mfupi kwani alianza kucheza bila kukata tamaa tangu mwaka 2017.
  ''Najua wengi mnaweza msiamini lakini mimi nilikuwa nacheza karibu kila wikiendi kuanzia mikeka 2 mpaka 5 nikiamini Ipo siku nitafanikiwa, Mungu mkubwa leo nipo mbele yenu natambulishwa kama mshindi wa Jackpot kubwa kabisa ya baba lao ya Sportpesa ya Tsh 1,255,316,060.
  Pesa hii Inakwenda kubadili maisha yangu kabisa na namuomba Mwenyezi Mungu niongoze Ili niweze kuizalisha zaidi na zaidi.
  “Niwaase watanzania wenzangu kuwa msikate tamaa na mcheze na Sportpesa kama mimi bila kukosa. Najua kuna wengine hawakucheza wikiendi ambayo mimi nimeishinda na hivyo mtakuwa mnajilaumu. Huwezi jua lini ni zamu yako. Hivyo napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Sportpesa kwa fursa ya ushindi na kuwa bilionea kupitia Jackpot''.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BILIONI 1.2 ZA JACKPOT YA SPORTPESA ZAENDA KILUVYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top