// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAYELE AFUNGA, YANGA YAITANDIKA MBEYA KWANZA 4-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAYELE AFUNGA, YANGA YAITANDIKA MBEYA KWANZA 4-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Friday, May 20, 2022

  MAYELE AFUNGA, YANGA YAITANDIKA MBEYA KWANZA 4-0


  VIGOGO, Yanga SC wamejisogeza jirani mno na ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Mbeya Kwanza usiku huu Uwanj wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na Fiston Mayele dakika ya 33, Said Ntibanzonkinza dakika ya 38, Dickson Ambundo dakika ya 45 na ushei na Heritier Makambo dakika ya 73.
  Yanga SC inafikisha pointi 63 katika mchezo wa 25 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 13 zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao wamecheza mechi 24, wakati Mbeya Kwanza inaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 ikibaki na pointi zake 21 za mechi 25 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE AFUNGA, YANGA YAITANDIKA MBEYA KWANZA 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top