• HABARI MPYA

  Saturday, May 14, 2022

  SIMBA SC YAIFUATA YANGA NUSU FAINALI ASFC  MABINGWA watetezi, Simba SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pamba FC ya Mwanza usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na viungo Mmalawi, Peter Banda dakika ya 45 na wazawa, Kibu Dennis mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya 48 na Yussuf Mhilu mawili, dakika ya 53 na 89.
  Simba SC itamenyana na watani wa jadi, Yanga katika Nusu Fainali, wakati Azam FC itamenyana na Coastal Union.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIFUATA YANGA NUSU FAINALI ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top