• HABARI MPYA

  Wednesday, May 11, 2022

  SIMBA SC YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-0 DAR


  MABINGWA watetezi, Simba SC wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba yamefungwa na washambuliaji wake wa Kimataifa wa Tanzania, Kibu Dennis dakika ya 13 na Nahodha, John Bocco dakika ya 29 wote wakimalizia pasi za kiungo Mzambia, Rally Bwalya.
  Kwa ushindi huo, Simba was SC inafikisha pointi 49, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nane na watani wao, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 23, wakati Kagera inabaki na pointi 29 mechi 23 nafasi ya saba.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Polisi Tanzania imelazimishwa sare ya bila kufungana na Dodoma Jiji FC Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkaoni Kilimanjaro, wakati Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga bao la Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 59 limewapa wenyeji, Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara United.
  Polisi inafikisha pointi 26, ingawa inashukia nafasi ya 11, ikiipisha Coastal nafasi ya 10 ambayo imefikisha pointi 27, Dodoma Jiji inafikisha pointi 28 na kusogea nafasi ya nane na Biashara inayobaki na pointi zake 23 sasa ni ya 13 baada ya wote kucheza mechi 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top