KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baina ya watani, Simba na Yanga ni Sh. 10,000 Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Taarifa ya TFF imesema viingilio vingine ni Sh, 30,000 VIP A na Sh, 20,000 VIP B na mchezo utaanza Saa 9:30 Alasiri.
0 comments:
Post a Comment