• HABARI MPYA

  Monday, May 09, 2022

  RASMI, DTB NI TIMU YA LIGI KUU MSIMU UJAO


  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeithibitisha klabu ya DTB ya Dar es Salaam kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu unaitwa, 2022-2023.
  Hiyo ni baada ya DTB kufikisha pointi 65 kileleni mwa Championship, tatu zaidi ya Ihefu inayofuatia na nane zaidi ya Kitayosce inayoshika nafasi ya tatu kuelekea mechi mbili za nwisho.
  Timu mbili za juu Championship zitapanda Ligi Kuu moja kwa moja na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Ligi Kuu kuwani kupanda.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RASMI, DTB NI TIMU YA LIGI KUU MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top