• HABARI MPYA

    Thursday, May 05, 2022

    GWIJI WA UFARANSA, TREZEGUET KUMLETA MWALI WA QATAR 2022


    MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, David Trezeguet anatarajiwa kuwasili nchini na Kombe halisi la Dunia la FIFA Mei 31, mwaka huu.
    Kwa mara ya nne mfululizo Tanzania imefanikiwa kuwa kati ya nchi 9 za Afrika ambazo kombe la Dunia litakuja nchini.
    Akizungumza jana katika uzinduzi wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Coca cola nchini, Unguu Sulay alisema kwa mara nyingine Tanzania imefanikiwa kupata tiketi ya kulishuhudia kombe hilo kabla ya kuelekea nchini Qatar katika fainali za mwaka huu.
    Sulay alisema ziara hiyo ni muendelezo wa kampuni yao kurudisha kiu na mipango ta Tanzania katika kusaka tiketi ya kushiriki kwa mara ya kwanza fainali hizo katika miaka ya baadaye.
    "Sio kila Taifa linapata hii nafasi,Tanzania imekuwa ni tofauti tumepata nafasi hii kwa mara ya nne kulipokea kombe hili halisi na watu kupata nafasi ya kupiga nalo picha," alisema Sulay.





    "Kombe hili litakuwa hapa nchini kwa siku mbili kuanzia Mei 31 na Juni Mosi na huu ni muendelezo wa kampuni yetu sio tu kuishia kuburudisha kupitia vinywaji bora lakini pia kujihusisha na moja kwa moja na msisimko wa kimichezo kupitia soka na burudani.
    Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa, robo tatu ya Watanzania wanapenda michezo na ziara hii inakuja kuwapa fursa watu wengi wenye rika tofauti kushuhudia kombe hili ambalo Tanzania inafanikisha ndoto za kuandaa fainali hizi.
    "Serikali na wizara yetu ya michezo imefarijika na ziara hii ikiwezeshwa na ninyi Coca cola, Rais wetu (Samia Suluhu Hassan) anapenda michezo na tuna ndoto za siku moja tuje kuandaa fainali hizi ingawa kwanza tunatakiwa kuamini inawezekana na baada ya hapo tujenge miundo mbinu kama vile viwanja," alisema Mchengerwa.... 
    Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia alisema ziara hii ya kombe hili ni muendelezo wa ushirikiano bora kati ya kampuni hiyo na TFF katika maendeleo ya mpira.
    " Coca cola imekuwa na mkono mzuri katika kuendeleza soka, sijui kama watu wanafahamu timu yetu ya Taifa Stars ya sasa ina wachezaji wengi ambao walizalishwa na mkakati wa kuzalisha vijana uliodhaminiwa na kampuni hii na ukaleta matunda bora kwa Taifa letu,"alisema Karia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GWIJI WA UFARANSA, TREZEGUET KUMLETA MWALI WA QATAR 2022 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top