• HABARI MPYA

    Tuesday, May 24, 2022

    AZAM FC YATOA SARE 1-1 NA RUVU SHOOTING MLANDIZI


    WENYEJI, Ruvu Shooting wamelazimishwa sare ya 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
    Elias Maguri alianza kuifungia Ruvu Shooting dakika ya 82, kabla ya Rodgers Kola kuisawazishia Azam Fc dakika ya 90.
    Azam FC inafikisha pointi 37, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa tu wastani wa mabao na Namungo FC inayoshika nafasi ya tatu, wakati Ruvu sasa ina pointi 28 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 26.
    Mechi iliyotangulia lao, bao pekee la Vincent Abubakar dakika ya 46 limeipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Coastal inafikisha pointi 34 na kusogea nafasi ya nne, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake 32 nafasi ya nane baada ya wote kucheza mechi 26 pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YATOA SARE 1-1 NA RUVU SHOOTING MLANDIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top