• HABARI MPYA

  Sunday, May 08, 2022

  LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA SPURS ANFIELD


  WENYEJI, Liverpool wamepunguzwa kasi katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Tottenham Hotspur Uwja wa Anfield.
  Son Heung-min alianza kuifungia Spurs dakika ya 56, kabla ya Luis Diaz kuisawazishia Liverpool dakika ya 74.
  Liverpool inafikisha pointi 83 katika mechi ya 35 na kupanda kileleni ikiizidi bao moja tu Manchester City yenye mechi moja mkononi na Jumapili inaikaribisha Newcastle United pale Etihad.
  Tottenham Hotspur yenyewe kwa sare hiyo inatimiza pointi 62 katika mechi ya 35, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi moja na Arsenal ambayo pia ina mechi moja mkononi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA SPURS ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top