• HABARI MPYA

  Wednesday, May 04, 2022

  LIVERPOOL YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA


  LIVERPOOL imefanikiwa kwenda Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Villarreal katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali usiku wa Jumanne Uwanja wa de la Cerámica mjini Villarreal nchini Hispania.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Fabinho dakika ya 62, Luis Díaz dakika ya 67 na Sadio Mané dakika ya 74 baada ya Villarreal kutangulia kwa mabao ya Boulaye Dia dakika ya tatu na Francis Coquelin dakika ya 41.
  Liverpool inafanikiwa kwenda Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-2 kufuatia ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani, England wiki iliyopita.
  Mechi ya mwisho ya marudiano ya Nusu Fainali ya UEFA Champions League inachezwa Jumatano usiku Hispania pia, baina ya wenyeji Real Madrid na Manchester City ya England Poa.
  Mchezo wa kwanza Manchester City inayofundishwa na kocha Mspaniola, Pablo Franco Martin ilishinda 3-2 Uwanja wa Etihad.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top