• HABARI MPYA

  Friday, May 13, 2022

  SPURS YAICHAPA ARSENAL 3-0 LONDON


  WENYEJI, Tottenham Hotspur wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Alhamisi Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
  Mabao ya Spurs yamefungwa na Harry Kane mawili, dakika ya 22 kwa penalti na 37 akimalizia pasi ya Rodrigo Bentancur na lingine Son Heung-Min dakika ya 47.
  Kwa ushindi huo, Spurs inafikisha pointi 65, ingawa inabaki nafasi ya tano, ikizidiwa 
  pointi moja moja na Arsenal baada wa wote kucheza mechi 36.
  Arsenal ilimaliza pungufu baada ya Rob Holding kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 33 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kucheza rafu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SPURS YAICHAPA ARSENAL 3-0 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top