• HABARI MPYA

  Tuesday, May 17, 2022

  KICHUYA APIGA MBILI NAMUNGO YAILAZA BIASHARA 2-1

  TIMU ya Namungo imewachapa wenyeji, Biashara United mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Mabao ya Namungo FC yote yamefungwa na Shiza Ramadhani Kichuya dakika ya tisa na 67, wakati la Biashara United limefungwa na Ambroce Awio dakika ya 85.
  Namungo FC inafikisha pointi 36 na kupanda nafasi ya tatu, ikiizidi pointi mbili Geita Gold baada ya wote kucheza mechi 24, wakati Biashara United inabaki na pointi zake 23 za mechi 24 sasa ikishukia nafasi ya 13.
  Ligi Kuu inashirikisha jumla ya timu 16 na mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KICHUYA APIGA MBILI NAMUNGO YAILAZA BIASHARA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top