• HABARI MPYA

  Wednesday, May 18, 2022

  LIVERPOOL YAICHAPA SOUTHAMPTON 2-1 ST MARY’S


  TIMU ya Liverpool imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya wenyeji, Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St Mary's .
  Southampton walitangulia na bao la Nathan Redmond dakika ya the 13, kabla ya Liverpool kuzinduka kwa mabao ya Takumi Minamino dakika ya 27 na Joel Matip dakika ya 67.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 89, ingawa inaendelea kushika nafasi ya pili nyuma ya Manchester City wenye pointi moja zaidi baada ya wote kucheza mechi 37.
  Southampton yenyewe inabaki na pointi zake 40 za mechi 37 nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA SOUTHAMPTON 2-1 ST MARY’S Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top