• HABARI MPYA

  Monday, May 23, 2022

  SABABU ZA AISHI KUMUACHIA LANGO BENO JANA KIRUMBA


  KIPA namba moja wa Simba, Aishi Salum Manula hakuweza kushiriki mechi ya jana ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Geita Gold Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa sababu ya ajali ndogo aliyopata.
  Taarifa ya Simba imesema dakika chache kabla ya kuanza kwa mchezo wa jana dhidi ya Geita Gold FC, Aishi Manula aliumia mkono baada ya kukatwa na kioo katika chumba cha kubadilishia nguo (dressing room).
  Manula aliwasili uwanja wa CCM Kirumba akiwa kwenye orodha ya wachezaji waliotakiwa kushiriki mchezo huo na baada ya kuingia katika chumba cha kubadilishia nguo akaangukiwa na kioo ambacho kilivunjika kufuatia kuegemewa na mashabiki waliokua nje chumba hicho. 
  Kipa namba mbili, Beno Kakolanya ndiye aliyedaka jana Simba ikitoa sare ya 1-1 na Geita.
  Tayari Aishi amepatiwa matibabu na anaendelea vizuri kuelekea mechi zijazo za kumalizia msimu ikiwemo dhidi ya watani, Yanga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SABABU ZA AISHI KUMUACHIA LANGO BENO JANA KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top