• HABARI MPYA

  Saturday, May 07, 2022

  MTIBWA YAICHAPA MBEYA CITY 1-0, GEITA GOLD YANG'ARA


  BAO la Said Hamisi Ndemla dakika ya 16 limeipa Mtibwa Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 22 na kusogea nafasi nane, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake 28 za mechi 22 sasa nafasi ya sita.
  Mechi iliyotangulia Geita Gold imeichapa Kagera Sugar 1-0, bao la George Mpole dakika ya tano Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 31 na kupanda nafasi ya tatu ikiizidi pointi moja Namungo FC baada ya wote kucheza mechi 22, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake 29 za mechi 22 sasa nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA YAICHAPA MBEYA CITY 1-0, GEITA GOLD YANG'ARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top