• HABARI MPYA

  Sunday, May 08, 2022

  SIMBA SC YAITANDIKA RUVU SHOOTING 4-1 DAR


  MABINGWA watetezi, Simba SC wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba yamefungwa na Kibu Dennis dakika ya 39, Rally Bwalya dakika ya 66, Nahodha John Bocco dakika ya 81 na beki Inonga Baka ‘Varane’ dakika ya 85, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Haroun Athumani Chanongo akiiadhibu timu yake ya zamani dakika ya 83.
  Simba inafikisha pointi 46, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi 10 na watani, Yanga baada ya wote kucheza mechi 22 kuelekea mechi nane za kukamilisha msimu.
  Hali ni mbaya kwa Ruvu Shooting baada ya kupoteza mechi ya leo 22, wakilingana kila kitu na Tanzania Prisons hadi mechi za kucheza, 22 na wastani wa mabao, wote wamefungwa mabao 11 zaidi ya waliyofunga na wanashika nafasi za 14 na 15, wakiizidi pointi moja tu Mbeya Kwanza inayoshika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAITANDIKA RUVU SHOOTING 4-1 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top