• HABARI MPYA

  Sunday, May 15, 2022

  YANGA SC YAZINDUKA, YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 JAMHURI


  VIGOGO, Yanga SC wamezinduka baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
  Ushindi huo wa kwanza katika mechi nne umetokana na mabao ya kiungo Dickson Ambundo dakika ya 11 akiiadhibu timu yake ya zamani na kipa Mohamed Yussuf aliyeudondeshea mpira langoni mwake katika harakati za kuokoa shuti la Zawadi Mauya dakika ya 35.
  Yanga inafikisha pointi 60 katika mechi ya 24 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi 11 zaidi ya mabingwa watetezi, Simba ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 28 za mechi 24 nafasi ya 10 sasa.


  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo zote zimeisha kwa sare ya 0-0, Mtibwa Sugar na Coastal Union Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro na Mbeya City dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mtibwa sasa ina pointi 28 nafasi ya nane, Coastal pointi 28 pia nafasi ya tisa, Mbeya City pointi 32 nafasi ya nne na Polisi Tanzania pointi 27 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 24 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAZINDUKA, YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top