• HABARI MPYA

  Friday, May 13, 2022

  AMBULANCE YAVUNJA MECHI YA NAMUNGO NA MBEYA KWANZA ILULU


  MECHI ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya wenyeji, Namungo FC na Mbeya Kwànza iliyopangwa kufanyika leo Saa 10:00 jioni Uwanja wa Ilulu mjini Lindi haikufanyika kutokana na kukosekana kwa gari la kubebea wagonjwa uwanjani hapo.
  Kiutaratibu mwenyeji wa mchezo ndiye anayepaswa kuhakikisha gari la wagonjwa lipo uwanjani kabla ya kuanza kwa mchezo na kukosekana kwa gari hilo mchezo hauwezi kuchezwa.
  Baada ya jitihada zilizofanywa na klabu ya Namungo magari mawili ya kubebea wagonjwa  yalifika uwanjani hapo mwendo wa saa 10:24 dakika sita kalba ya muda wa kikanuni wa kusubiri kwa dakika 30 kumalizika.
  Klabu ya Mbeya Kwànza iligomea kuendelea na  mchezo huo kwa madai kuwa muda wa kusubiria gari la wagonjwa ulikuwa umepita ambapo jitihada za kushawishi kufanyika kwa mchezo huo ziligonga mwamba. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMBULANCE YAVUNJA MECHI YA NAMUNGO NA MBEYA KWANZA ILULU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top