• HABARI MPYA

  Thursday, May 26, 2022

  YANGA YAWASIMAMISHA NTIBANZOKIZA NA AMBUNDO


  KLABU ya Yanga imewasimamisha wachezaji wake wawili, Dickson Ambundo na Mrundi Saido Ntibanzokiza kuelekea mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya watani, Simba SC Jumamosi Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Viungo hao washambuliaji wanadaiwa kutoroka kambini Jumatatu usiku mara baada ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Biashara United hapo hapo Kirumba anbayo iliisha kwa sare ya 1-1.
  Na kwa kosa hilo, kocha Mtunisia Nasredin Mohamed Nabi aliamuru warejeshwe Dar es Salaam wakati Yanga inakwenda kambini Shinyanga.
     


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAWASIMAMISHA NTIBANZOKIZA NA AMBUNDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top