• HABARI MPYA

  Friday, May 20, 2022

  CHELSEA YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA LEICESTER DARAJANI


  WENYEJI, Chelsea wamelazimishwa sare ya 1-1 na Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Leicester City ilitangulia na bao la James Maddison dakika ya sita, kabla ya Marcos Alonso kuisawazishia Chelsea dakika ya 34.
  Kwa sare hiyo, Chelsea inafikisha pointi 71, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikiizidi pointi tatu Tottenham Hotspur baada ya wote kucheza mechi 37, wakati Leicester City inafikisha pointi 49 za mechi 37 pia nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA LEICESTER DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top