• HABARI MPYA

  Tuesday, May 10, 2022

  MBEYA CITY YAICHAPA AZAM FC 2-1 SOKOINE


  WENYEJI, Mbeya City wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Mbeya City leo yamefungwa Juma Shemvuni dakika ya 51 na beki Mghana, Daniel Amoah aliyejifunga dakika ya 83 na la Azam limefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 88.
  Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 23 na kupanda nafasi ya nne, ikiizidi wastani wa mabao tu Geita Gold ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 32 za mechi 23 sasa nafasi ya tatu.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAICHAPA AZAM FC 2-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top