• HABARI MPYA

    Sunday, May 08, 2022

    COASTAL UNION YAICHAPA POLISI 1-0 MKWAKWANI


    WENYEJI, Coastal Union wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
    Bao pekee la Coastal Union limefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 21 na kwa ushindi huo Wagosi wa Kaya wanafikisha pointi 24 katika mchezo wa 22 na kupanda nafasi ya 12 kutoka mkoani.
    Polisi Tanzania inabaki na pointi zake 25 za mechi 21 nafasi ya 10.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA POLISI 1-0 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top