• HABARI MPYA

    Thursday, May 19, 2022

    KMC YAITANDIKA MBEYA CITY 3-0 UHURU

    WENYEJI, KMC wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya KMC yamefungwa na Awesu Awesu dakika ya 13, Matheo Anthony dakika ya 24 na Hassan Kabunda dakika ya 58.
    Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 25 na kusogea nafasi ya nane, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake 32 za mechi 25 nafasi ya sita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KMC YAITANDIKA MBEYA CITY 3-0 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top