• HABARI MPYA

  Wednesday, May 25, 2022

  POLISI TANZANIA YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0


  WENYEJI, Polisi Tanzania wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Mabao ya Polisi Tanzania yamefungwa na Datius Peter dakika ya 42 kwa penalti na Tariq Simba dakika ya 84.
  Kwa ushindi huo, Polisi Tanzania inafikisha pointi 30 na kusogea nafasi ya 11, ikiizidi pointi mbili Mtibwa Sugar baada ya wote kucheza mechi 26.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Mbeya Kwanza imeichapa Kagera Sugar 2-0, mabao ya Eliuter Mpepo dakika ya 51 na Jimmy Shoji dakika ya 58 Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
  Mbeya Kwanza inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 26 na kusogea nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, ikiizidi tu wastani wa mabao Tanzania Prisons ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Kagera Sugar baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 33 za mechi 26 nafasi ya saba.
  Ikumbukwe timu mbili zitashuka moja kwa moja mwishoni mwa msimu na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwani kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top