• HABARI MPYA

  Sunday, May 15, 2022

  MAN CITY YAAMBULIA SARE KWA WEST HAM, 2-2 LONDON


  MABINGWA watetezi, Manchester City wamelazimisha sare ya 2-2 na wenyeji, West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa London Jijini London.
  West Ham walitangulia kwa mabao ya Jarrod Bowen dakika ya 24 na 45, kabla ya Man City kuchomoa kupitia kwa Jack Grealish dakika ya 49 na Vladimír Coufal aliyejifunga dakika ya 69. 
  Manchester City ingeweza kuondoka na pointi zote tatu kama mshambuliaji Mualgeria, Riyad Mahrez angefunga penalti dakika ya 86, ambayo iliokolewa na Fabianski. Penalti hiyo ilifuatia Gabriel Jesus kuangushwa na Craig Dawson kwenye boksi.
  Man City inafikisha pointi 90 katika mchezo wa 37 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Liverpool ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi, wakati West Ham sasa ina pointi 56 za mechi 37 nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAAMBULIA SARE KWA WEST HAM, 2-2 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top