• HABARI MPYA

  Friday, May 13, 2022

  SIMBA SC YAMPA MAPUMZIKO MORRISON HADI MSIMU UJAO


  KLABU ya Simba imetangaza kumpa mapumziko winga wake Mghana, Bernard Morrison hadi mwishoni mwa msimu ili atatue matatizo ya kifamilia yanayomsibu kwa sasa.
  Na winga huyo wa zamani wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini ameandika katika ukurasa wake wa Instagram; “Kwa moyo mzito natangaza kwamba sitakuwepo kwa muda uliosalia wa msimu huu kwa sababu ya masuala ya kifamilia ambayo yapo nje ya uwezo wangu yanaweza kuathiri utendaji wangu katika timu ikiwa nitaendelea kuwa katika klabu. Mengi yanahitaji kusemwa kuhusu hilo, lakini naitakia klabu kila la kheri katika michezo yetu iliyosalia. Natumai na ninaomba nitatue hili haraka iwezekanavyo ili nijrejee kwenye timu‘“.
  Baada ya mchezo dhidi ya watani, Yanga uliomalizika kwa sare ya 0-0, Morisson aliyecheza kipindi cha kwanza pekee alifikishwa Polisi kwa tuhuma za kumchoma na kitu chenye ncha kali shabiki wa timu yake hiyo ya zamani nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMPA MAPUMZIKO MORRISON HADI MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top