• HABARI MPYA

  Monday, May 16, 2022

  KAGERA SUGAR YAICHIMBIA KABURI PRISONS


  WENYEJI, Tanzania Prisons wamechapwa bao 1-0 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Bao pekee la Kagera Sugar katika mchezo wa leo limefungwa na beki mkongwe, David Luhende dakika ya 88 na kwa ushindi huo, wanafikisha pointi 32 na kusogea nafasi ya tano, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 23 nafasi ya 15 baada y wote kucheza mechi 24.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, wenyeji, Ruvu Shooting wamelazimishwa sare ya 1-1 na KMC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Ruvu walitangulia na bao la mshambuliaji wake mkongwe, Fully Zulu Maganga dakika ya 19, kabla ya kiungo Awesu Awesu kuisawazishia KMC dakika ya 88.
  Ruvu wanafikisha pointi 26 nafasi ya 13 na KMC sasa wana pointi 28 nafasi ya nane baada ya wote kucheza mechi 24.
  Jumla ya timu 16 zinashiriki Ligi Kuu na mwisho wa msimu mbili zitateremka moja kwa moja na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHIMBIA KABURI PRISONS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top