• HABARI MPYA

  Sunday, September 05, 2021

  BIASHARA UNITED WAANZA SAFARI YA DJIBOUTI

   KIKOSI cha Biashara United ya Mara kinatarajiwa kutua Dar es Salaam kesho tayari kwa safari ya Djibouti kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika.
  Biashara iliyokuwa imeweka kambi Jijini Mwanza itashuka Uwanja wa El Hadj Hassan Gouled Jijini Ville de Djibouti ijumaa ijayo kumenyana na wenyeji, FC Dikhil, kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 18 hapa Dar es Salaam.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED WAANZA SAFARI YA DJIBOUTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top