• HABARI MPYA

  Friday, March 29, 2024

  MSIBA SIMBA SC, SHABIKI AFARIKI AJALINI AKIJA KUSHUHUDIA MECHI NA AHLY


  KLABU ya Simba imepata msiba baada ya shabiki wake mmoja kufariki ajalini akiwa safarini na wenzake kuja Dar es Salaam kushuhudia mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.
  Simba SC watakuwa wenyeji wa mabingwa hao watetezi katika mchezo huo wa kwanza wa Robó Fainali leo kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Timu hizo zitarudiana Aprili 5 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo, Misri na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali.
  Ikumbukwe timu hizo zilikutana katika Robó Fainali ya michuano mipya, African Football League na kutoa sare ya jumla ya 3-3, wakifungana 2-2 Oktoba 20 Dar es Salaam na 1-1 Oktoba 24 Cairo, hivyo Al Ahly kwenda Nusu Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini.


  Watani wao, Yanga SC wameguswa na msiba huo na kuwapa pole Simba.
  Yanga nao watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns kesho kuanzia Saa 3:00 usiku pia Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana  Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria.
  Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2001 na Mamelodi Sundowns wakaitoa Yanga kwa jumla ya mabao 6-5, wakishinda 3-2 Pretoria na kutoa sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mshindi wa jumla baina ya Yanga na Mamelodi Sundwons atakutana na mshindi wa jumla katí ya Esperance ya Tunisia na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSIBA SIMBA SC, SHABIKI AFARIKI AJALINI AKIJA KUSHUHUDIA MECHI NA AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top