• HABARI MPYA

  Wednesday, March 06, 2024

  AZAM FC YAAMBULIA SARE KWA COASTAL UNION 1-1 CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Unión katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Coast al Union walitangulia kwa bao la Charles Semfuko dakika ya 68, kabla ya kiungo mwenzake, Feisal Salum Abdallah kuisawazishia Azam FC dakika ya 81.
  Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 44 katika mchezo wa 20 na kurejea kileleni ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi nne mkononi.
  Kwa upande wao Coastal Unión sare ya leo inawafanya wafikishe pointi 27 katika mchezo wa 19, ingawa wanabaki nafasi ya nne wakizidiwa pointi tisa na Simba SC ambayo pia ina mechi tatu mkononi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAAMBULIA SARE KWA COASTAL UNION 1-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top