• HABARI MPYA

  Saturday, March 02, 2024

  SIMBA SC YATINGA TENA ROBÓ FAINALI LIGI YA MABINGWA KWA KISHINDO


  WENYEJI, Simba SC wamefanikiwa kutinga Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mchezo wa mwisho wa Kundi B leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Wekundu wa Msimbazi yamefungwa na kiungo Mrundi, Saido Ntibazonkiza dakika ya saba, mshambuliaji Mgambia, Pa Omar Jobe dakika ya 14, viungo mzawa, Kibu Denis Prosper dakika ya 22, Mzambia Clatous Chotta Chama dakika ya 76, mzawa Ladack Juma Chasambi dakika ya 86 na Mkongo Fabrice Luamba Ngoma dakika ya 89.
  Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi B, wenyeji, Wydad Casablanca wameshinda 1-0 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast bao pekee la kiungo mzawa, Mountassir Lahtimi dakika ya 18 Uwanja wa Marrakech, Morocco.
  Simba SC inamaliza na pointi tisa sawa na Wydad Casablanca, wote wakiwa nyuma ya vinara, ASEC Mimosas wenye pointi 11.
  Wekundu wa Msimbazi wanatinga Robó Fainali kwa faida ya ushindi wa jumla dhidi ya Wydad kufuatia kufungwa 1-0 Morocco na kushinda 2-0 Dar es Salaam na pia wanastawisha kufuzu kwao kwa wastani mkubwa zaidi wa mabao zaidi ya timu ya Casablanca.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATINGA TENA ROBÓ FAINALI LIGI YA MABINGWA KWA KISHINDO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top