• HABARI MPYA

  Saturday, March 02, 2024

  KAGERA SUGAR SARE 1-1 NA JKT TANZANIA KAITABA


  WENYEJI, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  JKT Tanzania walitangulia na bao la Edward Songo dakika ya 22, kabla ya Mubarak Hamza kuisawazishia Kagera Sugar kwa penalti dakika ya 41.
  Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya saba na JKT Tanzania inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 18 ingawa inabaki nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR SARE 1-1 NA JKT TANZANIA KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top