• HABARI MPYA

  Friday, March 01, 2024

  YANGA SC WAMALIZA MAKUNDI NA KICHAPO CHA 1-0 KWA AHLY


  TIMU ya Yanga imekamilisha mechi zake za Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa 1-0 na wenyeji, Al Ahly usiku huu Uwanja wa Venue Cairo International Jijini Cairo nchini Misri.
  Bao pekee la mabingwa hao watetezi limefungwa na kiungo mkongwe Mmisri Hussein El Shahat dakika ya 46 akimalizia pasi ya beki Mtunisia, Ali Maâloul.
  Mechi nyingine ya Kundi D leo wenyeji, CR Belouizdad wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Medeama SC ya Ghana, mabao ya Abdelraouf Benguit dakika ya 27, Leonel Wamba dakika ya 42 na Lamin Jallow dakika ya 84 Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers.
  Al Ahly inamaliza kileleni mwa Kundi D kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na Yanga pointi nane na zote zinafuzu Robó Fainali, wakati CR Belouizdad iliyomaliza na pointi nane pia ikizidiwa wastani wa mabao na Yanga na Medeama SC iliyomaliza na pointi nne zote safari yao inaishia hapa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAMALIZA MAKUNDI NA KICHAPO CHA 1-0 KWA AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top