• HABARI MPYA

  Sunday, March 17, 2024

  BONDIA WA TANZANIA AMCHAKAZA MSHELISHELI NA. KUTINGA ROBÓ FAINALI ALL AFRICAN GAMES  Ezra (Mwenye jezi ya Blue) baada ya kutangazwa rasmi mshindi wa pambano hilo la leo.

  BONDIA Ezra Paulo Mwanjwango amefanikiwa kutinga Robó Fainali ya Michezo ya Afrika (All African Games) inayoendelea nchini Ghana baada ya kumshinda kwa RSC (Refa Kusimamisha Pambano) William Mohamed wa Shelisheli 
  Ilikua katika round ya pili, Dk ya 2 na Sekunde 38 ambapo Kamanda huyo wa Kikosi cha Faru Weusi wa Ngorongoro aliweza kuwainua mashabiki wake kwa kumaliza pambano hilo kwa RSC, refa akisitisha pambano kumuokoa na kipigo zaidi mpiganaji wa Shelisheli.
  Bondia mwingine wa Tanzania Abdallah Mafaume ‘Nachoka’ ametolewa na Gerald Kabinda wa Zambia kwa pointi 5-0 uzito wa Welter Hatua ya 16 Bora.
  Anakuwa bondia wa pili wa Tanzania kutolewa baada ya Abdallah Abdallah ‘Katoto’ aliyelazimika kujiuzulu juzi katika raundi ya mwisho akipigana na Wibshet Bekele wa Ethiopia kufuatia kuvunjika mkono, ingawa alikuwa anaongoza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BONDIA WA TANZANIA AMCHAKAZA MSHELISHELI NA. KUTINGA ROBÓ FAINALI ALL AFRICAN GAMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top