• HABARI MPYA

  Monday, March 25, 2024

  YANGA NA MAMELODI SUNDOWNS MACHI 30 NI ‘MUDA DAY’ MTAMBO WA MABAO JANGWANI


  KLABU ya Yanga imeamua mchezo wake wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns Machi 30 Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam utapewa heshima ya kiungo wao mzawa, Mudathir Yahya Abbas ‘Muda Day’.
  Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Shaaban Kamwe amesema kwamba tayari Mudathir Yahya na wachezaji wengine wawili, beki Ibrahim Hamad ‘Bacca’ na mshambuliaji, Clement Francis Mzize waliokuwa na timu ya taifa nchini Azebairjani wamerejea na kujiunga na timu.
  Kuhusu wachezaji wanaosumbuliwa na maumivu, Kamwe amesema beki Kibwana Shomari, viungo Zawadi Mauya na Mganda Khalid Aucho wanaendelea vizuri na mazoezi na mashaka bado yapo kwa nyota wa Ivory Coast, beki Kouassi Attohoula Yao na kiungo Peodoh Pacôme Zouzoua.
  Yanga watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns Jumamosi ya Machi 30 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana  Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria.
  Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2001 na Mamelodi Sundowns wakaitoa Yanga kwa jumla ya mabao 6-5, wakishinda 3-2 Pretoria na kutoa sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mshindi wa jumla baina ya Yanga na Mamelodi Sundwons atakutana na mshindi wa jumla katí ya Esperance ya Tunisia na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
  GONGA KUTAZAMA VÍDEO ALLY KAMWE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA MAMELODI SUNDOWNS MACHI 30 NI ‘MUDA DAY’ MTAMBO WA MABAO JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top