• HABARI MPYA

  Friday, March 15, 2024

  NI MAN CITY NA REAL MADRID, ARSENAL NA BAYERN MUNICH ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA


  MABINGWA watetezi, Manchester City ya England watamenyana na mabingwa wa kihistoria, Real Madrid ya Hispania katika Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Katika droo ya michuano hiyo iliyopangwa leo Jijini Nyon, Uswisi, vinara wa Ligi Kuu England, Arsenal watamenyana na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich, wakati 
  Atletico Madrid ya Hispania itacheza na Borussia Dortmund ya Ujerumani na bingwa wa Ufaransa, PSG  ataumana na Barcelona ya Hispania pia.
  Nusu Fainali zitakutanisha mshindi kati ya Atletico Madrid na Borussia Dortmund na mshindi kati ya PSG na Barcelona na mshindi kati ya Arsenal na Bayern Munich dhidi ya mshindi kati ya Real Madrid na Manchester City.
  Mechi za kwanza za Robó Fainali zitachezwa Aprili 9 na 10 na marudiano yatafuatia April 16 na 17, wakati Nusu Fainali za kwanza ni Aprili 30 na Mei 1 na marudiano ni May 7 na 8, wakati Fainali ni Juni 1 Uwanja wa Wembley Jijini London.
  RATIBA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA:
  Arsenal vs Bayern Munich
  Atletico Madrid vs Borussia Dortmund
  Real Madrid vs Manchester City
  PSG vs Barcelona
  NUSU FAINALI:
  Atletico Madrid/Borussia Dortmund v PSG/Barcelona
  Arsenal/Bayern Munich v Real Madrid/Manchester City
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI MAN CITY NA REAL MADRID, ARSENAL NA BAYERN MUNICH ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top