• HABARI MPYA

  Monday, March 25, 2024

  BEKI WA ZAMANI SIMBA NA YANGA, RAMAZANI WASSO AFARIKI DUNIA


  BEKI wa zamani wa Kimataifa wa Burundi, Ramazani Wasso amefariki dunia leo kwa Bujumbura nchini Burundi baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda.
  Wasso alijiunga na Simba SC mwaka 2001 na alikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichoitoa kwa penalti Zamalek ya Misri baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003.
  Wasso alihamia kwa watani, Yanga mwaka 2004 baada ya kuwahadaa Simba anakwenda Ubelgiji kucheza soka ya kulipwa, ingawa mwaka 2007 alirejea Msimbazi na kucheza hadi 2009 akahamia Coastal Unión ya Tanga kumalizia soka yake.
  Mungu ampumzishe kwa amani Ramazani Wasso.
  GONGA KUTAZAMA MAHOJIANO YA WASSO NA BIN ZUBEIRY ENZI ZA UHAI WAKE 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI WA ZAMANI SIMBA NA YANGA, RAMAZANI WASSO AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top