• HABARI MPYA

  Friday, March 08, 2024

  YANGA YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA NAMUNGO FC 3-1


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Mabao ya Yanga leo yamefungwa na wazawa, kiungo Mudathir Yahya Abbas dakika ya 54, mshambuliaji Clement Francis Mzize dakika ya 57 na kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki dakika ya 62, huku bao pekee la Namungo FC akijifunga beki mzawa, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ dakika ya 69.
  Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha pointi 46 katika mchezo wa 17 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu wakiizidi pointi mbili Azam FC ambayo pia imecheza mechi tatu zaidi.
  Kwa upande wao Namungo FC baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 23 za mechi 20 sasa nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA NAMUNGO FC 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top