• HABARI MPYA

  Friday, March 22, 2024

  TANZANIA YAAMBULIA MEDALI TATU ZA SHABA NDONDI ALL AFRICAN GAMES


  MATOKEO ya kushangaza ya Majaji usiku wa jana yalimnyima Ushindi Nahodha wa Timu ya Taifa Yusuf Changalawe baada ya kupoteza kwa points katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Pita Kabeji kutoka DR Congo katika michezo ya Afrika Accra 2023 inayoendelea nchini Ghana.
  Ilikuwa katika uzani wa Light Heavyweight 80kg ambapo Changalawe alicheza kwa ustadi wa hali ya juu lakini cha kushangaza maamuzi ya Majaji yakampa ushindi mpinzani wake Pita Kabeji. 
  Matokeo hayo yamemuudhunisha sana Changalawe aliyejiwekea dhamira ya kuwa Bingwa wa Afrika katika uzani huo.
  Wakati huohuo bondia mwingine Musa Maregesi wa uzani wa Cruiserweight 86kg naye haikua siku nzuri kazini baada ya kupoteza pia katika hatua hio ya nusu fainali dhidi ya Kanouni O. kutoka Algeria kwa points 5-0. 
  Safari ya ngumi ndio imeishia hapo ambapo sasa Tanzania imejihakikishia kupata medali 3 za Shaba kutoka katika mchezo wa ngumi za Yusuf Changalawe, Musa Maregesi  na Ezra Paulo Mwanjwango.
  _"Hakika ni mwanzo mzuri wa kujivunia mafanikio haya ya kuanzia mwaka 2024, tumeendelea vizuri pale tulipoishia mwaka jana wa 2023"_......alinukuliwa Raisi wa Shirikisho la Ngumi Tanzania Ndg. Lukelo Willilo.
  Ngumi mwaka 2023 ilifanikiwa kupata medali 3 kutoka katika Mashindano ya Ubingwa wa Afrika Yaounde 2023, Cameroon medali 2 (1 ya Fedha ya Grace Mwakamele na Shaba ya Yusuf Changalawe) na katika mashindano ya kufuzu kushiriki Olimpiki ya Paris 2024 kwa Bara la Afrika medali 1(Fedha ya Yusuf Changalawe)
  Mwaka 2022 pia ngumi ilifanikiwa kupata medali 2 za Shaba katika mashindano ya Jumuiya ya Madola ya Birmingham 2022 kwa mabondia Yusuf Changalawe na Kassim Mbundwike.
  Mafanikio yote chanya yametokana na ushirikiano wa karibu na Serikali ya Awamu ya Sita hususani uwezeshaji wa Timu za Taifa unaoendelea kufanywa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan pamoja na wadau wote walioshiriki kuchangia harambee ya kuwezesha timu za Taifa.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YAAMBULIA MEDALI TATU ZA SHABA NDONDI ALL AFRICAN GAMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top