• HABARI MPYA

  Sunday, March 24, 2024

  ITABA ACHAPWA KWA TKO RAUNDI YA KWANZA ENGLAND


  BONDIA Hussein Itaba wa Tanzania usiku wa jana amepigwa na mwenyeji, Liam Cameron kwa Technical Knockout (TKO) Raundi ya kwanza katika pambano la Raundi sita uzito wa Light Heavy ukumbi wa Sheffield Arena, Sheffield, England.
  Katika pambano hilo lililoandaliwa na promota maarufu, Muingereza Eddie Hearn - refa Reece Carter wa Wales alimaliza mchezo baada ya Hussein Itaba kuangushwa mara mbili katika Raundi hiyo ya kwanza.
  Itaba jana alipigana pambano la pili ndani ya siku nane Uingereza, baada ya Machi 16 kupoteza kwa pointi mbele ya mwenyeji mwingine, Thomas O'Toole ukumbi wa Salthill Leisureland Complex, Galway nchini Ireland pambano lililondaliwa na Kampuni ya MHD Promotions.
  Baada ya kupigana vizuri siku hiyo, MHD Promotions wakavutiwa na Itaba na kumuumganishia pambano la jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ITABA ACHAPWA KWA TKO RAUNDI YA KWANZA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top