• HABARI MPYA

  Monday, March 11, 2024

  YANGA SC YAITANDIKA IHEFU 5-0 NA KUJIWEKA HURU KILELENI LIGI KUU


  MABINGWA watetezi, Yanga wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuitandika Ihefu SC mabao 5-0 leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga leo yamefungwa na viungo yote, Muivory Coast Peodoh Pacôme Zouzoua dakika ya 10, mzawa Mudathir Yahya Abbas dakika ya 30, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 68, Mghana Augustine Okrah dakika ya 84 na Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 85.
  Kwa ushindi huo mtamu, Yanga ya Kocha Muargentina Miguel Ángel Gamondi inafikisha pointi 49 katika mchezo wa 18 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya Azam FC ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi.
  Kwa upande wao Ihefu SC baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 23 za mechi 20 sasa na kushuka kwa nafasi moja hadi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAITANDIKA IHEFU 5-0 NA KUJIWEKA HURU KILELENI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top