• HABARI MPYA

  Saturday, March 23, 2024

  AZAM FC YAWACHAPA ZIMAMOTO 2-1 MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI


  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Zimamoto ya Zanzíbar katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na mawinga wake hatari, Muivory Coast Kipre Tiagori Emmanuel Junior Zunon dakika ya 10 na Iddi Suleiman Nado kwa penalti dakika ya 59.
  Kwa upande wao Zimamoto bao lao pekee la katika mchezo huo limefungwa na mshambuliaji Ibrahim Hamad Ahmada ‘Hilika’ dakika ya 28.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWACHAPA ZIMAMOTO 2-1 MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top